Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi, James Mbatia
KAMBI
Rasmi ya Upinzani Bungeni kupitia kwa Waziri Kivuli wa Fedha na Uchumi,
James Mbatia, imesoma bajeti mbadala wa ile iliyowasilishwa na Serikali,
huku ikiainisha masuala kadhaa ya kukuza uchumi na kupunguza
utegemezi...Anaandika Mwandishi Wetu ... (endelea).
Kwa
mujibu wa Mbatia aliye Mbunge wa Kuteuliwa na Mwenyekiti wa Taifa wa
NCCR-Mageuzi, katika kipindi cha miezi minne ijayo kuanzia sasa,
Serikali ya CCM ianze kujiandaa kisaikolojia kuondoka madarakani na
kupiisha kwa amani serikali adilifu itakayoongozwa na UKAWA kuingia
madarakani ili waweze kuwatumikia Watanzania.
Akiwasilisha
maoni ya upinzani leo kwa Bajeti ya 2015/16, Mbatia amesema
“tunapendekeza kukusanya Sh. bilioni 19,695.2 ambapo mapato ya kodi na
yasiyo ya kodi Sh. bilioni 18,847.1 (sawa na asilimia 20) ya Pato la
Taifa.”
No comments:
Post a Comment