AU yaamua kutuma haraka wataalam wa kijeshi Burundi
Hali ya hofu imeendelea kutanda mjini Bujumbura, Burundi.
Umoja wa
Afrika umeendelea kutiwa wasiwasi na hali ya kisiasa na usalama nchini
Burundi, baada ya mazungumzo ya kisiasa kusimama ghafla, huku mpatanishi
wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro wa Burundi, Said Djinnit akijiuzulu
kufuatia ombi la vyama vikuu 17 vya upinzani na mashirika ya kiraia
yanayopinga muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza.
Katika
mkutano wa kilele wa 25 wa Umoja wa Afrika (AU) jijini Johannesburg
Jumapili Juni 14, Umoja huo umeamuaa " kupelekwa haraka timu ya
waangalizi wa Haki za Binadamu na wataalamu wa kijeshi kutoka Umoja wa
Afrika na Umoja wa Ulaya watakaosimamia mchakato wa kuwapokonya silaha
wanamgambo pamoja na makundi mengine yenye silaha nchini Burundi ",
Smail Chergui, Kamishna wa Amani na Usalama, ametangaza Jumatatu Juni
15.
Hayo
yanajiri wakati ujumbe wa jumuiya ya nchi za Afrika Mashariki umewasili
tangu Jumapili usiku mjini Bujumbura. Ujumbe huo unaoundwa na mawaziri
wa mambo ya nje wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekutana Jumatatu wiki
hii na rais Pierre Nkurunziza na vyama vikuu vya upinzani.
No comments:
Post a Comment