Mkurugenzi Mkuu wa Twitter, Dick Costolo anayetarajia kujiuzulu.
Mkurugenzi
Mkuu wa Twitter, Dick Costolo, ana nia ya kujiuzulu ifikapo Julai mosi,
kufuatia shinikizo kutoka kwa wawekezaji, ambao wanalalamikia kukua
polepole wa mtandao huo wa kijamii.
Baada ya kujiuzulu nafasi hiyo ya Mkurugenzi Mkuu, Costolo atabaki kuwa Mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa kampuni hiyo.
Twitter imeshindwa kupata faida katika kipindi cha miaka tisa tangu ilipoanzishwa.
Mwanzilishi
mwenza wa mtandao huo Jack Dorsey anatarjiwa kuchukua nafasi hiyo kama
kaimu Ofisa Mkuu kuanzia Julai mosi na kukalia wadhifa huo hadi pale
mrithi wake atakapochaguliwa.
Katika taarifa yake, Costolo amesema kuwa anafurahishwa na wafanyikazi wa kampuni hiyo.
Mnamo
mwezi Aprili kampuni hiyo ilipata hasara ya dola milioni 162 hivyo
kufanya ukuaji wa kampuni kushuka kwa kiwango kikubwa na kuathiri
uwekezaji.
Bei ya hisa zake ilishuka kwa asilimia 30 na sasa zinaendelea kuuzwa kwa bei ya uanzilishi wake ya mwaka 2013
No comments:
Post a Comment