Friday, June 12, 2015

WAZIRI MKUU, MIZENGO PINDA ACHUKUA FOMU YA URAIS


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akichukua fomu za urais mkoani Dodoma leo.
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda leo amechukua fomu ya kuwania kugombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mhe. Pinda amechukua fomu hiyo katika makao makuu ya chama hicho yaliyopo mkoani Dodoma ambapo pia alipata fursa ya kuongea na wanahabari.
Katika mkutano wake na wanahabari amekataa kuelekezea mengi kama walivyofanya watangaza nia wenzake ili kutoingilia ilani ya chama chake.
Asema ana uzoefu wa uongozi na mafanikio yote ya wizara nchini yeye ndiye kiranja wake.
Apanga kuongeza ukuaji wa uchumi wa pamoja ili kuondoa umbali kati ya mwenye nacho na asiyekuwa nacho.

No comments:

Post a Comment