Friday, June 12, 2015

Monica Mbega: Ikulu ni zamu yangu wengine wasindikizaji



Monica Mbega (kulia) akifurahi pamoja na wana CCM Iringa mjini ambao walijitokeza kumdhamini kuwa mgombea wa nafasi ya urais kupitia CCM WAKATI mbio za makada wa chama cha mapinduzi (CCM) waliotia nia ya kuomba kuteuliwa kuwa wagombea wa nafasi za urais zikiendelea kushika kasi kwa kila mgombea kutumia mbinu yake ya kuwafikia wana CCM kuomba udhamini , aliyekuwa mbunge wa jimbo la Iringa mjini Monica Mbega leo ameingia wilaya ya Iringa Mjini mkoani hapa kuomba udhamini na kupata wajumbe 33 huku akiwataka watanzania kutoaminishwa na mbwembwe za watia nia wenzake wanazofanya mikoani na kuwa yeye ndie Rais wa awamu ya tano baada ya Dk Jakaya Kikwete na kuwataka watia nia wenzake wamuunge mkono.

Mbega ambae alilazimika kusubiri wajumbe 30 wa kumdhamni kwa zaidi ya masaa manne katika ofisi ya CCM wilaya ya Iringa mjini alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanahabari juu ya safari yake hiyo ya kutaka kwenda Ikulu na kudai kuwa amelazimika kuzuia viongozi wa CCM wilaya ya Iringa kutomuandalia mbwembwe zozote wala wapambe wa kumshangilia wakati wa safari yake hiyo ya kutafuta wadhamini.
Alisema kuwa kuwa anamtegemea Mungu zaidi katika safari yake hiyo ya kwenda Ikulu na ndio maana hakupenda kuweka makisio ya gharama za safari nzima ya mchakato huo wa kuelekea kupokea kijiti kwa Rais Dk Kikwete na hivyo ndio sababu ya yeye kuzunguka bila ya mpambe zaidi ya dereva anayemuendesha pekee.

No comments:

Post a Comment