Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Maritim Hotel Bw.Wissmann
katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani jana alipowasili katika Mji huo
akiwa katika ziara ya Kiserikali ambapo atahudhuria ufunguzi wa maonesho
ya Muziki yanayojumuisha wasanii kutoka nchi za Afrika na Mabara
mengine (kulia) Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Philip Marmo, [Picha
na Ramadhan Othman.]
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na
Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakisalimiana na Wazanzibari waliofika
kuwapokea mara walipowasili Maritim Hotel katika Mji wa Wurzburg Nchini
Ujerumani wakiwa katika ziara ya kiserikali pamoja na ujumbe wa Viongozi
mbali mbali aliofuatana nao katika ziara hiyo inajumuisha na maonesho
ya Muzikiyanayojumuisha Wasanii mbali wa Nchi za Afrika na Mabara
mengine ambayo hufanyika kila mwaka,
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa ZIPA Nd,Salum Khamis Nassor mara
walipowasili Maritim Hotel katika Mji wa Wurzburg Nchini Ujerumani akiwa
na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (kushoto) wakiwa katika ziara ya
kiserikali Nchini humo,ambapo atatembelea Sehemu kadhaa za kihistoria na
Kiuchumi.
No comments:
Post a Comment