Friday, June 12, 2015

TFF YATOA OFA 'BAB KUBWA' KWA WAZAZI WA SIMON MSUVA


Rais wa TFF Jamal Malinzi akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa tuzo jana usiku
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kupitia kwa Rais wake Jamal Malinzi, jana usiku lilitoa ofa kwa wazazi (baba na mama) wa Simon Msuva kuhudhuria mechi mbili za timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ itakapokuwa ikicheza dhidi ya Uganda kwenye michezo ya awali kuwania kufuzu kushiriki michuano ya Afrika inayoshirikisha wachezaji wa ligi za ndani (CHAN).

Malinzi ametoa ofa hiyo kwa wazazi wa Msuva ambaye jana alitangazwa kuwa mchezaji bora wa ligi kuu ya soka Tanzania bara iliyomalizika Mei 9 mwaka huu ikiwa kama zawadi na shukrani kwa wazazi hao mara baada ya wazazi wa Msuva kueleza njia ndefu aliyopita mtoto wao kufikia mafanikio anayoyapata hivisasa na wao kusimama nyuma yake kwa kila jambo gumu na rahisi alilopitia kijana wao. 
Baba yake Simon Msuva (mzee Msuva) akiwa ameinua juu tuzo ya mfungaji bora wa ligi iliyokwenda kwa Simon Msuva, (kulia kwake) ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia na (kushoto kwake) ni mama yake Simon Msuva
Baba yake Simon Msuva (mzee Msuva) akiwa ameinua juu tuzo ya mfungaji bora wa ligi iliyokwenda kwa Simon Msuva, (kulia kwake) ni Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Juma Nkamia na (kushoto kwake) ni mama yake Simon Msuva.

No comments:

Post a Comment