Kupitia kwa mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani Klaus Allofs amethibitisha kwa mshambuliaji wa zamani wa Chelsea kurudi katika Ligi Kuu Uingereza. Klaus Allofs amethibitisha kuwa klabu ya Wolfsburg imeridhia kumuachia Kevin De Bruyne ajiunge na klabu ya Manchester City.
Kevin De Bruyne atakuwa anarejea katika Ligi Kuu Uingereza ikiwa ni miezi 18 imepita toka aondoke katika Ligi hiyo akitokea klabu ya Chelsea na kujiunga na klabu ya Wolfsburg.
“Tutamaliza
kila kitu aidha usiku huu au kesho De Bruyne yupo njiani kujiunga na
Manchester City nilizungumza katika Press siku ya jumanne kuwa bado
tulikuwa tunaendelea na mazungumzo,mazungumzo yalikuwa yakiendelea hadi
sasa imebakia sehemu ndogo sana kumalizana”>>> Klaus Allofs
Kevin De Bruyne alianza kucheza soka professional akiwa katika klabu ya Genk mwaka 2008. Alisajiliwa na klabu ya Chelsea January mwaka 2012 kabla ya kurudishwa kwa mkopo katika klabu yake ya Genk, baada ya hapo aliendelea kucheza kwa mkopo katika klabu ya Werder Bremen ambapo aliichezea mechi 33 za Bundesliga na kufunga magoli 10.
Mshambuliaji huyo anarudi Uingereza kwani hadi anaondoka Chelsea katika msimu wa 2013-2014 alicheza mechi tatu pekee na kuuzwa katika klabu ya Wolfsburg kwa ada ya pound milioni 18 mwezi January 2014. Inaripotiwa kuwa ndani ya masaa 24 au 48 De Bruyne atakuwa amejiunga na klabu ya Man City kwa ada ya uhamisho ya pound milioni 54.
No comments:
Post a Comment