Mgombea
wa urais kupitia CCM, Dk John Magufuli ameendelea kumwaga ahadi mikoa
ya Katavi na Rukwa na kuahidi kuwa iwapo atachaguliwa kuwa rais wahudumu
wanaoiba dawa katika hospitali nchini watakiona cha moto.
Akiwahutubia
wakazi wa Namanyere mkoani hapa leo, Dk Magufuli alisema anataka
kutengeneza nchi isiyo na kero ikiwemo kuondoa tatizo la uhaba wa dawa.
Mgombea
huyo, ambaye jana aliingia siku ya pili kuzunguka mikoani kuomba kura,
alisema tabia ya watu kwenda hospitali kutibiwa na kuambiwa wakanunue
dawa kwenye maduka kwa kuwa vituo vya afya havina dawa, ataikomesha.
"Nafahamu
kuna matatizo ya dawa kwenye hospitali eti ukienda kutibiwa unaandikiwa
cheti ukanunue dawa mahali pale, sasa pale wamepataje hizo dawa?" alihoji.
"Wale wote wenye tabia ya kuiba kuiba dawa, madaktari, ili wapeleke sehemu nyingine, moto wao unakuja."
Alisema
akingia madarakani atahakikisha dawa zinapatikana kila hospitali na ili
kutatua tatizo la wizi wa dawa ataboresha masilahi ya madaktari na
manesi.
Dk
Magufuli ambaye muda wote amekuwa akiwataka wananchi wamwamini kwa
ahadi zake, alisema siku zote anachukia rushwa, uzembe, na manyanyaso
kwa wengine huku baadhi wakifaidi rasilimali za nchi.
No comments:
Post a Comment