Polisi yamtahadharisha Lowassa staili ya kampeni zake
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtahadharisha mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema Edward Lowassa kuwa kampeni alizoanza kwa kuyatembelea makundi kadhaa zinaweza kutumiwa na maadui wa kisiasa kumdhuru.
Hata
hivyo, wanasiasa wametakiwa kufuata ratiba ya kampeni kwa kuzingatia
mwongozo wa Tume ya Uchaguzi (NEC) ili kulisaidia jeshi hilo kukabiliana
na vitendo viovu.
Onyo
hilo limetolewa ikiwa ni siku ya pili tangu Lowassa na mgombea mwenza
Juma Duni Haji walipoanza kuwatembelea wananchi huku wakitumia usafiri
wa umma.
Kwa kutumia staili hiyo, leo Lowassa akiwa na Duni Haji wametembelea maeneo ya Tandika, Tandale na Kariakoo jijini Dar.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dar, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar es
Salaam, Suleiman Kova amesema ziara iliyofanywa leo maeneo ya Swahili,
Kariakoo zimesababisha mikusanyiko isiyo ya lazima na kusimamisha
shughuli za maendeleo.
Baada
ya CCM kuzindua kampeni zake mwishoni mwa juma lililopita viwanja vya
Jangwani, jijini Dar es Salaam, Chadema nacho kinajiandaa kufanya hivyo
Agosti 29 maeneo hayohayo.
No comments:
Post a Comment