Aliyekuwa mpenzi wa mshambuliaji wa kiitaliano na klabu ya AC Milan ya Italia Mario Balotelli kwa sasa ameamua kuingia katika mahusiano ya kimapenzi na staa mwingine wa soka. Balotelli aliacha na Fanny Neguesha mwezi Septemba mwaka jana baada ya kutokuwa katika maelewano mazuri kati yao.
Mrembo Fanny Neguesha kwa sasa ameingia katika headlines na staa mwingine wa soka kutokea Senegal anayeichezea klabu ya West Ham United ya Uingereza Cheikhou Kouyate. Stori ilianza wiki iliyopita baada ya West Ham United kushinda goli 4-3 dhidi ya Bournemouth, hivyo mrembo huyo alipost picha Instagram akiwa amevaa jezi namba 8 ya staa huyo hivyo watu wakaanza kuhoji ukaribu wao.
No comments:
Post a Comment