Sio siri kuwa foleni za airport huwa
zinakera wakati mwengine haswa ukiwa unataka kusafiri kutoka mji moja
kwenda mwengine na ndio maana wenzetu wa Marekani wanaona suluhisho la tatizo hili ni ‘Vertical Take Off and Landing Airplanes (VTOLs)’ peke yake.
Kampuni ya XTI VTOLs Aircraft iliyopo Marekani wamekuja na njia mpya ya usafiri wa anga, chombo chenye muonekano wa ndege na helicopter kwa wakati mmoja kisichohitaji uwanja kupaa wala kutua na chenye uwezo wa kukufuata moja ka moja nyumbani kwako!
VTOLs TriFan600 ni miongoni mwa ndege hizi zenye uwezo wa kupaa na kutua haraka kama Helicopter, uwezo wa kuwabeba abiria kutoka majumbani kwao, mahotelini mwao na kuwasafirisha mpaka pale wanapotaka kwenda!
Wenyewe wanasema huu utakuwa ‘usafiri wa mlango kwa mlango’
kwani unatengenezwa kuboresha safari za anga ndani ya nchi… so pata
picha unafatwa na ndege hii nyumbani kwako mtu wangu na inakupeleka moja
kwa moja Mwanza au Arusha bila kutumia uwanja wa ndege wa Mwl. Nyerere, ingekuaje!?
Mwenyekiti wa XTI Aircraft, Jeffery Pino amesema usafiri wa ‘mlango kwa mlango’ Marekani umeonekana kuwa na uhitaji mkubwa kutokana na hali kwenye viwanja vya ndege kubadilika kadri siku zinavyoenda, hivyo anatumaini TriFan600 na zingine zitakuwa mwanzo wa kutatua au suluhisho la tatizo hili.
Matoleo mengine yanayotarajia kuja chini ya kampuni hii ni haya hapa chini..
No comments:
Post a Comment