Afriyie Acquah amecheza na Jordan Ayew katika timu ya taifa ya Ghana toka mwaka 2012 lakini kuvuja kwa Audio ambayo inaripotiwa ni sauti ya Amanda mke wa Afriyie Acquah akikiri kuwa katika mahusiano na Jordan Ayew kwa miaka minne inaweza kuleta chuki kati yao.
“Nimekuwa
na mahusiano ya kimapenzi na Jordan kwa miaka minne na sio siku nne,
alikuwa akinitumia picha za utupu, ametembea na mimi zaidi ya Acquah
tumekuwa katika mahusiano pamoja hadi kufikia kuwa kama mke na mume
“>>> Amanda
Jordan Ayew amejiunga na klabu ya Aston Villa msimu huu akitokea klabu ya Lorient ya Ufaransa kwa ada ya pound milioni 8 na amesaini mkataba wa miaka mitano ila kupitia kwa msemaji wa klabu ya Aston Villa jibu la Jordan ni kuwa klabu haiwezi kuingilia maisha binafsi ya mchezaji.
Hivyo tukio hili linaweza kuwafanya wote
wakakosa kuitwa timu ya taifa au mmoja wao akaachwa kwani ni ngumu kuwa
na wachezaji ambao wapo timu moja sema hawaongei kwa mujibu wa vyanzo
vya karibu na watu hao Jordan alikuwa hapendi kuongea na Acquah ila Andre Ayew ambaye ni kaka wa Jordan walikuwa wakiongea.
No comments:
Post a Comment