Mapendekezo
hayo wameyatoa baada ya kusikia hali tete inaoukabili mkoa wa Manyara
unaoonekana kuwekwa kwenye alama nyekundu iliyo hatarishi kwenye
mazingira ya vifo hivyo hapa nchini,hasa pale ilipobainika kuwa hata
huduma jumuishi kwenye mazingira ya vijijini hazina tija sambamba na
kiwango cha watoto wanaozaliwa na akinamama wenye VVU na kupata dawa za
(ARV'S) za kufubaza VVU hazifiki hata asilimia 23 ya huduma na hatari
kwa vifo hivyo.
Nayee
mganga mkuu mkoani manyara Dr. Ali Bin Uledi katika taarifa yake kwa
wadau hao amekiri kuwepo kwa vifo 665 vya watoto chini ya umri wa miaka
mitano hadi kufikia mwaka 2014 vinavyochangiwa na uhaba wa huduma ya
uzazi wa mpango,watendaji kukosa weledi,na hakuna hospitali hata moja
yenye utaratibu wa kutoa dawa zenye kukomaza mapafu ya mtoto mtarajiwa
kwa mama aliyepatwa uchungu wa kujifungua.
Hata
hivyo mkuu wa mkoa wa manyara Dr.Joel Nkaya Bendera maarufu
kama"KOCHA"aliyeonekana kushtushwa na changamoto ya vifo hivyo huku mkoa
wake ukiwa kwenye kiashiria cha alama nyekundu amesema ingawa sababu
kubwa inayochangia ni kutowajibika kwa watendaji,lakini ni lazima sasa
kuwepo kwa jitihada za kupunguza vifo vya mama kutoka vifo 34 na vile
vya watoto kwa kila mmoja akiwajibika,kabla ya kugawa azimio la
uwajibikaji na mkakati.
No comments:
Post a Comment