mwanahabari
frank kibiki , aliyewahi kuwa katibu wa umoja wa vijana wa chama cha
mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya miaka 10 na ambaye ni
mjumbe wa nec akiwa na watoto waliofanyiwa ukaliti wa kijisia pamoja
mkuu wa kituo cha matumaini centre
mwandishi wa habari wa gazeti la mzalendo na uhuru TUMAINI MSOWOYA KIBIKI akiwa na watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia.(P.T)
mwandishi
wa habari wa gazeti la mzalendo na uhuru TUMAINI MSOWOYA KIBIKI akiwa
na watoto waliofanyiwa ukatili wa kijinsia pamoja na mkuu wa kituo cha
matumaini centre.
Na Fredy Mgunda,Iringa
Ukatili
wa kijinsia kwa watoto wa kike ndio inaonekana kuwa sababu ya mkoa wa
iringa kuzalisha wafanyakazi wengi wa kazi za ndani
akizungumza
na blog hii mwanahabari frank kibiki , aliyewahi kuwa katibu wa umoja
wa vijana wa chama cha mapinduzi (uvccm) ngazi ya wilaya kwa zaidi ya
miaka 10 na ambaye ni mjumbe wa nec.amesema kuwa watoto wengi wa kike
hawapewi nafasi ya kwenda kusoma kutokana na tamaduni potofu hivyo
waandishi wa habari tunatakiwa kuungana kuwapigania watoto hawa.
Aidha
KIBIKI amewataka wananchi wa mkoa wa iringa kushirikiana na mkuu wa
kituo cha matumaini centre ili kuwasaidia watoto wa kike ambao wanaishi
katika kituo hicho.
lakini
KIBIKI amewaomba viongozi mbalimbali na waandishi wa habari kupaza
sauti zetu ili kukomeshakabisha suala la ukatili wa kijinsia ambao bado
unaendelea hapa mkoani kwetu.
Wananchi
mkoani iringa wametakiwa kuwathamini na kuwapa elimu watoto wa kike ili
kupunguza unyanyasaji wa kijinsia unaoendelea kwa sasa.
Kwa
upande wake mkurugenzi kituo cha matumaini centre HELLEN NKUNDA amesema
kuwa amekuwa akipokea watoto wengi wa kike ambao wamefanyiwa ukatili wa
kijinsia na amekuwa akiwapokea na kuwapa elimu ya ufundi.
Lakini
NKUNDA amewataka watoto hao kuwa makini na waaminifu katika maisha yao
ili wasirudie yale ambayo yalimtokea hapo awali na wasikubari
kudanganywa tena.
NKUNDA
ameitaka serikali kutoa elimu kuanzia shule ya msingi juu madhara ya
ukatili ili kujenga jamii ambayo itakuwa na elimu juu ya unyanyasaji na
ukatili wa kijinsi hasa kwa watoto wa kike.
Alimalizia
kwa kumshukuru mwandishi wa habari frank kibiki kwa kutoa msaada wake
kwa mtoto ambaye aliyekuwa amefanyiwa ukatili wa kijinsia.
No comments:
Post a Comment