Marufuku Ya Vyama Kuwa Na Vikosi Vya Ulinzi Ni Ya Kuungwa Mkono
- Written by Mjengwa Blog
- Add new comment
Ndugu zangu,
Nianze kwa kumpongeza Msajili wa Vyama Vya Siasa na IGP kwa kulifanyia kazi hili la vyama vya siasa kuwa na vikosi vya ulinzi.
Ingawa
maamuzi ya kupiga marufuku yamekuja kwa kuchelewa, lakini, bado ni ya
kupongezwa na wote wenye mapenzi mema na nchi yetu tuliyozaliwa. Ni
maamuzi ya kuungwa mkono kwa nguvu zote.
Hakika,
yalikuwa ni makosa makubwa katika wakati tulio nao, kuruhusu vyama vya
siasa kujipa mamlaka ya kujiandalia vikosi vyake vya ulinzi kwenye nchi
yenye watu waliogawanyika inapohusu itikadi za vyama. Si busara pia,
kuacha makosa hayo yaendelee kufanyika, kwa vile tu, eti, vyama husika
vimeweka taratibu hizo za kuwa na vikosi vya ulinzi kwenye Katiba zao.
Kimsingi, vyama vyenye kupingana na marufuku hiyo vina mawili tu ya
kuchagua; Mosi, kurekebisha vifungu vya katiba vyao vyenye kuruhusu
kuundwa kwa vikosi vya ulinzi, au, kukubali Msajili avifute vyama hivyo.
Kwa hilo la mwisho, vyama vitakuwa na uhuru wa kwenda na vikosi vyao
msituni na kupambana na dola.(P.T)
Vinginevyo,
jukumu la kuhakikisha raia, bila kujali itikadi zao, wanahakikishiwa
Ulinzi na Usalama wao linabaki kuwa ni la Serikali Kuu kupitia Jeshi
lake la Polisi. Kama kuna mapungufu kwenye utekelezaji wa jukumu hilo,
basi, uwepo mjadala wa kulisemea hilo na hatua zichukuliwe. Na hapa
Serikali iangalie pia uwezekano wa kurefusha marufuku ya taasisi kuwa na
vikundi vyake vya ulinzi, kuwa ifike mpaka kwenye taasisi za kidini.
Hakika,
tunashukuru sana kwa Msajili na IGP kuitikia kilio cha wengi wetu
tuliokuwa tukipinga utaratibu wa vyama kuwa na vikosi vya ulinzi. Na
hapa nitakumbushia nilichoandika hapa Machi 4 kufuatia mahojiano
niliyofanyiwa na mtangazaji wa Zenj FM. Alitaka kupata maoni yangu juu
yanayoendelea nchini mwetu. Mtangazaji alianza kwa kuorodhesha
changamoto zinazozikabili taifa anazonitaka maoni yangu.
Nilimwambia,
kuwa muda wa kwenye radio ni mfupi kuzichambua changamoto hizo lukuki
zikaeleweka kwa wasikilizaji. Na nikamwambia, kuwa hata hizo
alizoziorodhesha ni chache.
Hata hivyo, nikamwomba mtangazaji nichambue changamoto moja kubwa ninayoiona mimi inalikabili taifa kwa sasa kuelekea Uchaguzi Mkuu. Kwamba inahusu USALAMA.
Hata hivyo, nikamwomba mtangazaji nichambue changamoto moja kubwa ninayoiona mimi inalikabili taifa kwa sasa kuelekea Uchaguzi Mkuu. Kwamba inahusu USALAMA.
Nilisema,
kwamba katika nchi yoyote iwayo, bila USALAMA kwa maana pia ya uwepo wa
Amani na Utulivu, basi, hakutakuwa na maendeleo ya kiuchumi.
Kuna ishara katika nchi yetu, kuwa baadhi ya wanasiasa tuliowapa dhamana za uongozi wanaonyesha kucheza kamari na Amani na Utulivu wetu kama Taifa. Wanachokifanya ni kamari yenye matokeo ya dhahiri, kuwa kama taifa, tutakwenda kupoteza tulicho nacho.Wahenga walisema; Majuto Ni Mjukuu. Burundi na Rwanda ni mfano wa nchi jirani tu zinazojutia hata hii leo kwa kufumbia macho tunachokiona sisi leo.

Kimsingi,
vinavyoitwa vikosi vya Ulinzi vya Vyama vya siasa ni moja ya kamari
mbaya inayochezwa na wanasiasa itakayopelekea maangamizi makubwa. Haya
ni mambo tuliyoiga tangu enzi za Ushoshalisti ambayo hata huko
yalikotokea wameyaacha.
Wakati umebadilika. Katika wakati tulio nao, vijana waandaliwe ' Ukakamavu' wa kiakili kuwa na uwezo wa kuelewa itikadi, sera, madhumuni na malengo ya vyama vyao. Wafanye hivyo ili waweze kuvinadi vyama vyao kwa wapiga kura. Kazi ya ulinzi iachwe kwa vikosi vinavyotambulika kisheria na kwa mujibu wa Katiba yetu.

Nchi ina
Amiri Jeshi Mkuu mmoja. Sasa hivi vikosi vya kivyama vinakula viapo vya
namna gani kwenye Jamhuri? Hivi hatujui maana ya viapo vya kijeshi?
Na hata majina ya vikosi hivi vya kiwanamgambo yanatia mashaka. Mathalan, hivi hatujui maana ya Red Brigades na chimbuko lake?
Na hata majina ya vikosi hivi vya kiwanamgambo yanatia mashaka. Mathalan, hivi hatujui maana ya Red Brigades na chimbuko lake?
Red
Brigades kilikuwa kikundi cha wanamgambo wenye itikadi kali za mrengo wa
kushoto za Ki-Marxist na Leninist kule nchini Italia. Kiliipata
umaarufu miaka ya 70 kwa matendo yake ya kutumia njia za utekaji nyara.
Mwaka 1970, Red Brigades ilifahamika zaidi kwa kufanikiwa kumteka nyara
na hatimaye kumwua aliyekuwa Waziri Mkuu wa Italia, Aldo Moro.
Na si wengi wenye kufahamu, kuwa ni mwaka ule 1978, Mnajimu Sheikh Yahya Hussein alipata umaarufu zaidi kwa kuaminika kuwa alitabiri tukio lile la Aldo Moro kutekwa nyara na Red Brigades. Ni kupitia utabiri wake mwanzoni mwa mwaka huo, kuwa mwaka huo wa 1978 unheshuhudia kiongozi mmoja mashuhuri akitekwa nyara.

Kwa
kuhitimisha, nikashauri kupitia mtangazaji yule wa Zenj FM, kuwa umefika
wakati wa Serikali kupiga marufuku ya uanzishaji na uendeshaji wa
vikundi hivi vya wanamgambo wa vyama. Vyama vya siasa viachwe kufanya
siasa, na Jukumu la Ulinzi liachwe kwa vyombo vya ulinzi vyenye
kutambulika kisheria na kikatiba. Neno langu la mwisho likawa;
Hatujachelewa.
Maggid,
Dar es Salaam.
Maggid,
Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment