Staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma.
MWANDISHI WETU
KUTOKANA
na matukio mabaya yanayomtokea staa wa filamu za Kibongo, Wastara Juma,
shehe aliyejulikana kwa jina la Shaban Ally wa jijini Dar, ameibuka na
kumuonya mwigizaji huyo kwamba kama anataka 'mabalaa' yasizidi
kumuandama basi arejee kwa Mungu wake kwani anaonekana amemuacha.
Shehe
huyo alifikia hatua hiyo kutokana na Wastara kuandamwa na ajali za mara
kwa mara kwani hivi karibuni alianguka chooni na kabla hajakaa sawa
akapata ajali ya gari na kuumia usoni.Shehe Shaban alisema staa huyo
anatakiwa kumrudia Mungu kwani kawaida kwa mtu anayetokewa na majanga
hayo kuna uwezekano mkubwa wa kuwa amebadili aina ya maisha kutoka
katika yale yanayompendeza na kuishi yale yanayomchukiza Mungu.
"Wastara
anatakiwa kumrudia Mungu wake, aachane na mambo ya duniani maana katika
dini ya Kiislamu, usiposwali unaweza kupatwa na majanga ya ajabu kila
kukicha kama hivi yanavyomtokea yeye," alisema shehe huyo
No comments:
Post a Comment