Wednesday, April 15, 2015

Mwanamuziki Percy Sledge aaga dunia

Percy Sledge nyakati zake Mwanamuziki chapa 'Soul' aliyetikisa ulimwengu kwa miaka mingi kutokana na utunzi wake ''When a Man Loves a Woman'',Percy Sledge ameaga dunia.

Raia huyo wa Marekani aliaga dunia akiwa na umri wa miaka 73 nyumbani kwake Baton Rouge, Louisiana.
Afisa wa muungano wa wasanii Steve Green, ameithibitishia BBC kifo cha muimbaji huyo nguli.
Wimbo wake uliovuma kote duniani kwa miaka na mikaka '' When a Man Loves a Woman'' uligonga orodha ya kumi bora mara mbili nchini Uingereza.

'' When a Man Loves a Woman'' uligonga orodha ya kumi bora mara mbili nchini Uingereza Sledge aliyewahi kuvuma katika runinga ya BBC Two mwaka wa 1994 kwa ushirikiano na Jools Holland alishikilia nafasi ya kwanza kwa majuma mawili mfululizo alipozindua wimbo huo''When a Man Loves a Woman'' mwaka wa 1966.
Muimbaji huyo pia alitesa sana nchini Uingereza wimbo wake huo ulipopanda hadi nafasi ya nne katika jedwali la kumi bora.
Na haikuishia hapo Percy Sledge, alirejea kwa kishindo mwaka wa 1987 alipotoa nakala ya wimbo huo na mara utunzi wake ukabobea kwa mara nyengine tena nchini Uingereza.
Wimbo huo ''When a Man Loves a Woman'' ulivuma na kuwa wapili kwa umaarufu nchini Uingereza.
Sledge alisherehekea miaka 49 tangu alipotangazia ulimwengu wa Muziki wa Soul kuwasili kwake na wimbo huo ''When a Man Loves a Woman''.

Sledge aliwahi kuwa muuguzi kabla ya kufuata talanta yake na kuibukia kuwa muimbaji hodari. Bwana huyo aliweka historia alipoandikwa katika daftari la wanamuziki waliobobea yaani '' Rock and Roll Hall of Fame katika mwaka wa 2005''.
Sledge alikuwa mwanachama wa muungano wa wanamuziki kutoka Alabama.(V.S)

No comments:

Post a Comment