Kijana aliyeokolewa baada ya kufunikwa na kifusi kwa siku tano wakati wa tetemeko la ardhi mjini Kathmandu.
Kufuatia
tetemeko kubwa la aridhi kuukumba Mji wa Kathmandu nchini Nepal siku
tano zilizopita, waokoaji wamefanikiwa kumuokoa kijana mmoja mwenye umri
wa miaka 15 aliyepatikana hai baada ya kufunikwa na vifusi vya jengo
alilokuwemo wakati wa tetemeko hilo.
Licha
ya kuwa chini ya maporomoko ya vifusi hivyo kwa siku tano, taarifa
zinasema kuwa kijana alisaidiwa na mwanya uliokuwa ukipenyeza hewa
iliyomwezesha kupumua japo kwa shida.
Makundi
ya watu walimshangilia alipotolewa huku akionekana akijitahidi kufungua
macho yake. Alikimbizwa hospitali mara moja kupata matibabu zaidi.
Zaidi ya watu 5,500 wamethibitishwa kufariki kutokana na janga hilo.
Wengi
wa wahanga hao wanasubiri misaada ya chakula na maji safi ya kunywa
huku mashirika ya kutoa misaada yakisema huenda ikachukua siku nyingine
tano kabla ya kuwafikia baadhi yao kutokana na kuharibiwa kabisa kwa
miundo mbinu.
Umoja
wa mataifa umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuendelea kutoa misaada
wakikadiria michango inayohitajika kuwa zaidi ya dolla millioni 415
kuisaidia Nepal katika kipindi cha miezi 3 ijayo
No comments:
Post a Comment