Mkuu wa
Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akikagua Mazingira ya Soko la
Mahakama ya Ndizi lililopo Mabibo akiwa ameambatana na Viongozi wa
wafanyabiashara wa soko hilo alipofika kusikiliza kilio chao. Mkuu wa
Wilaya ya Kinondoni Ametembelea Soko hilo baada ya viongozi wa soko hilo
kufikisha kilio chao cha muda mrefu kwake.
Mkuu wa
Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipatiwa Maelezo zaidi kuhusu eneo
la Soko hilo kutoka kwa Mwenyekiti wa Soko Hilo Ndugu Idd Pazi kwa
niaba ya Wafanyabiahara wa Soko Hilo.
Mkuu wa Wialaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akizungumza na wafanyabiashara wa soko la Ndizi lililopo Mabibo, akiwaambia amepokea kwa mikono miwili kilio chao na kwamba atalifanyaia kazi kwa haraka kwa kushirikiana na ngazi mbalimbali za maamuzi na mapema atawajibu.Mkuu wa Wilaya huyo amesema ni ngumu sana kwake kutoa ahadi ambayo itakuwa ngumu kutekelezeka kwa kuwa eneo hilo ni Mali ya Kiwanda cha Urafiki na kiwanda kimebinafsishwa hivyo ni ngumu kuahidi kama watalipata eneo hilo kwa ajili ya Soko Bila kujua Mipango ya Kiwanda kuhusu eneo hilo
No comments:
Post a Comment