Raia wa kigeni ashambuliwa Afrika Kusini
Kumekuwa na mashambulizi zaidi usiku dhidi ya biashara zinazomilikiwa na raia wa kigeni nchini Afrika Kusini.
Polisi
walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mipira kutawanya umati
kusini mwa mji wa Johannesburg ambapo gari na nyumba vilichomwa moto.
Msemaji
wa polisi aliiambia BBC kuwa karibu raia mia mbili wa kigeni
walikimbilia usalama kwenye kituo cha polisi lakini wakaondoka muda
baadaye.
Usalama umedumishwa kufuatia mashambulizi yaliyowalenga raia wa kigeni ambapo watu watano wameuawa.
Rais
Jacob Zua amelaani ghasia hizo na maandamano ya amani mjini Durban siku
ya Alhamisi yalihudhuriwa na zaidi ya watu elfu kumi
No comments:
Post a Comment