LICHA ya
mwenyewe kukanusha vikali lakini madai mazito yanasema kuwa, nyota wa
Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ametimuliwa kwenye nyumba aliyokuwa akiishi
iliyopo Kunduchi-Beach jijini Dar baada ya kukosana na mwanamke
anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake ambaye pia ndiye mmiliki wa mjengo huo.
Habari
kutoka kwa chanzo makini zinaeleza kuwa, pamoja na Kiba kuendelea
kusisitiza kwamba si kweli, mwanamke huyo anayeishi nchini Singapore,
aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kusoma kwenye mitandao ya kijamii
na vyombo vingine vya habari kuwa, kwa sasa Kiba anatoka na Miss
Tanzania namba 2, 2006, Jokate Mwegelo ëKidotií huku Kiba mwenyewe
akikataa madai hayo.
Mjengo ambao Ali Kiba anadaiwa kutimuliwa .
KISIKIE CHANZO (DK)
Hivi
jamani! Mnajua kuwa, Ali (Kiba) ametimuliwa kule Kunduchi-Beach kwenye
ile nyumba aliyowekwa na yule demu mwenye fedha zake na ndiye aliyekuwa
akimgharamia kila kitu?
Aliyemponza
ni yule Kidoti, Jokate Mwegelo. Jokate amekuwa akimposti Kiba kwenye
mitandao ya kijamii, ndipo mwanadada huyo alipoona akachukia na kumuona
Kiba ameshindwa kuthamini fadhila zake, kilidai chanzo hicho makini.
Jokate Mwegelo ‘Kidoti’.
ARUDI KWAO
Sasa hivi
amerudi kwa mama yake, Kariakoo (Dar) kutokana na yeye mwenyewe
kulikoroga kwa kuupiga teke mgodi wa fedha. Japokuwa mara kwa mara Kiba
mwenyewe amekuwa akikanusha kujihusisha kimapenzi na Jokate, lakini
ukweli ni kwamba ameshaharibu kwa mwanadada aliyekuwa anamuwezesha,î
kiliongeza chanzo hicho.
ALICHOKISEMA MTU WA KARIBU NA KIBA
Baada ya
kuvujishiwa nyeti hiyo, mapaparazi wetu walimtafuta mtu mmoja ambaye
yupo karibu sana na Mbongo-Fleva huyo ambaye hakutaka jina lichorwe
gazetini na kukiri kuwa, msanii huyo amehama Kunduchi-Beach, badala yake
amehamia mjini kwa muda katika kipindi cha Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa
Ramadhani.
Ni kweli
mshkaji (Kiba) sasa hivi haishi Kunduchi (Beach). Amehamia mjini
(hakutaka kusema mjini ipi) ambapo anakaa kwa kipindi kifupi tu kisha
atahamia kwenye makazi yake mapya maeneo ya Upanga (Dar) ambako
kunafanyiwa ukarabati, alisema mtu huyo.
ALI KIBA SASA
Katika
kuweka sawa mzani wa madai hayo, juzi mapaparazi wetu walimtafuta staa
huyo wa Ngoma ya Chekecha Cheketua kwa njia ya simu na kumuuliza kuhusu
madai hayo na kutaka kujua anakoishi hivi sasa, ambapo alifunguka hivi:
Unataka
kujua naishi wapi ili iweje? Wakati unajua kabisa kuna matatizo
yalinipata (kuvamiwa). Sasa nikisema si naweza kujitafutia matatizo
mengine?
Siwezi kusema ninapoishi kwa usalama wa maisha yangu na kuhusu huyo mwanamke ni maneno ya watu wenye lengo la kunichafua.
AMZUNGUMZIA JOKATE
Jokate ni
mwanamke ambaye nipo naye karibu katika vitu vingine ambavyo ni vya
msingi zaidi na si hivyo ambavyo watu wanahisi. Lakini kama kuna mtu
atahisi tofauti itakuwa juu yake. Mimi na Jokate ni washkaji ‘long time’
(muda mrefu) katika mambo kibao.
KUHUSU KUTIMULIWA KWENYE NYUMBA
Kuhusu
nyumba nilishawahi kufafanua kwamba siyo yangu. Kuna mtu aliniweka kwa
makubaliano maalum, lakini ninashangaa kusikia taarifa ambazo zipo
tofauti juu ya ukweli ambao mimi ninaufahamu.
TUJIKUMBUSHE
Miezi
kadhaa iliyopita kuliibuka utata juu ya umiliki wa nyumba hiyo baada ya
kudaiwa ni ya Kiba lakini uchunguzi wetu ukabaini siyo yake, naye
akakiri akidai kwamba alipanga
No comments:
Post a Comment