Wawakilishi
wa Kudumu wa Tanzania, Balozi Tuvako Manongi na Christopher Grima Malta
wakitia sahihi hati za kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia katika ngazi
ya Mabalozi. Wanaoangalia utiaji sahihi ni Tully Mwaipopo Afisa
Mwandamizi wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania na Bw. Alan Cordina,
Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Malta
Na Mwandishi Maalum, New York
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Malta zimekubaliana kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia baina yao.
Wawakilishi
wa Kudumu wa mataifa hayo mawili katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako
Manongi wa Tanzania na Christopher Grima wa Malta ndio waliotia sahihi
hati za kuridhia kuanzishwa kwa uhusiano huo na ambao utakuwa katika
ngazi ya Mabalozi.
Wakizungumza
mara baada ya utiaji sahihi hati hizo, wawakilishi hao wameelezea kuwa
kuanzishwa kwa uhusiano huo ni hatua muhimu sana katika kukuza na
kuendeleza ushirikiano na uhusiano kati ya mataifa hayo mawili na watu
wake.
Tanzania
imekuwa ikinufaika kwa ufadhili wa nafasi za masomo kutoka Malta kwa
watumishi mbalimbali wakiwamo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Kimataifa na Wizara nyingine.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi na Mwakilishi wa Kudumu wa Malta katika Umoja wa Mataifa, Balozi Christopher Grima wakipongezana mara baada ya kutia sahihi hati walizoshika za kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia katika ngazi ya Mabalozi. Hati hizo baadaye ya zitawasilishwa rasmi kwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
No comments:
Post a Comment