Tuesday, June 23, 2015

Mgombea Urais wa CCM aliyepigwa Tanga azungumza (Audio)


Kalokola
Moja ya video ambayo watu wameshare sana kwenye mitandao ya Kijamii hasa kwenyeWhatsapp siku chache zilizopita ilikuwa inaonesha Mgombea mmoja wa CCM akipigwa japo wengine waliiona hiyo video na hawakujua ni nani anayepiga na anapigwa kwa sababu gani !!

Magazeti yakaipa headlines tena hiyo ishu June 20 2015, Mgombea ambaye alipigwa akatajwa kwamba ni Dk. Mussa Muzamil Kalokola na sababu iliyoandikwa ni ishu ya kuingia kwenye Mkutano ambao hakuandaliwa yeye Tanga.
“Nilipigwa sana lakini msisikitike kuona mimi nimepigwa kwa sababu bwana Yesu alikufa msalabani kutuokoa sisi... nipigwe mie ili mafisadi wasichukue nchi hii wanaotembeza mitonyo kutaka kununua Urais wakati wao ndio wameangamiza nchi hii kwa kutuibia“ Dk. Kalokola
Kwani ni kweli alivamia Mkutano wa Mgombea mwingine?  “Sikuvamia.. nimeenda na Askari wao wenyewe katika Kamati ya Siasa wakaanza kuniomba radhi wananiambia yaishe”
Hapa anasimulia ilivyokuwa mpaka wakampiga “Nilikuwa naenda kwa Katibu wa Wilaya jamaa wakaanza kusema mwondoe mwondoe.. Jamaa akanifuata nikampa teke maana na mimi nimepita Jeshini katika Kung-fu na mimi nipo... walivoona nimewazidi nguvu akaja kijana mwingine akanipiga ngwala... nimeumia miguu”Dk. Kalokola
Hapa akasikika Nape Nnauye akizungumzia ishu hiyohiyo  “Sijui nani mkosaji japokuwa hata kama yeye alikuwa amevamia kitendo cha kumpiga vile haikuwa sawa... Hata kama imetokea bahati mbaya wamekutanishwa sehemu moja bado kumpiga haikuwa sawasawa” Nape Nnauye
Sauti ya Dk. Kalokola na Nape Nnauye ziko hapa, utawasikia wote wawili ukiplay!!

No comments:

Post a Comment