MKURUGENZI
Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti Magonjwa ya Binadamu Dk Mwele
Malecela mtoto wa Makamu wa zamani wa CCM John Malecela ni miongoni mwa
wana CCM ambao wamejitosa kugombea urais kupitia CCM.
Dk Mwele
kesho amepangiwa na CCM kuchukua fomu za kuomba kugombea urais. Ratiba
ya CCM iliyotolewa jana Makao Makuu ya chama hicho mjini hapa inaonesha
kuwa licha ya Dk Mwele, mwingine ambaye atachukua fomu hiyo kesho ni
Nicholaus Mtenda ambaye pia amejitokeza kuomba kugombea urais kupitia
CCM.
Dk Mwele
katika maisha yake mengi kwa zaidi ya miaka 20 amekuwa mtumishi katika
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) ambako
alianza kazi akiwa kijana na akapanda hadi kuwa mtafiti mkuu na baadaye
akateuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu.
Licha ya
kukulia katika familia ya mwanasiasa maarufu nchini, lakini Dk Mwele
hajawahi kujitokeza hadharani kushiriki kwenye masuala ya siasa. Kama
akichukua fomu hiyo kesho, atakuwa ni mwanamke wa pili kuomba kuteuliwa
na CCM kugombea urais kumrithi Rais Jakaya Kikwete.
Mwanamke
mwingine ni Balozi Amina Salum Ali wa Zanzibar. Jana Waziri wa Malisili
na Utalii, Lazaro Nyalandu na wanachama wengine wawili wa CCM walichukua
fomu za kuwania urais. Nyalandu alikuwa wa kwanza kufika katika ofisi
za CCM kuchukua fomu akiwa amefuatana na familia yake na wafuasi wake
kadhaa
No comments:
Post a Comment