Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimvisha
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro Nishani ya Jamhuri ya Muungano
Daraja la Kwanza kwa kuwa mwaminifu na kujitolea moja kwa moja kulipatia
Taifa sifa kubwa katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiulinzi na
kijamii wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu
leo Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akimvisha
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Liberata Rutegaruka Mulamula Nishani ya Jamhuri ya Muungano Daraja la
Kwanza kwa kuwa mwaminifu na kujitolea moja kwa moja kulipatia Taifa
sifa kubwa katika Nyanja za kisiasa, kiuchumi, kiulinzi na kijamii
wakati wa sherehe zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu leo
Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akimvisha
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Florens Martin Turuka Nishani
ya Utumishi mrefu na Maadili mema Daraja la kwanza kwa kuwa mtumishi wa
umma kuanzia ngazi ya ukurugenzi na kutumikia Taifa si chini ya ishirini
mfululizo na kuonyesha maadili mema wakati wa sherehe zilizofanyika
kwenye ukumbi wa Mikutano Ikulu leo Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment