Sunday, June 21, 2015

MAONESHO YA UTALII YA SANGANAI ZIMBABWE YAFUMBUA MACHO WATANZANIA


IMG_4145
Pichani juu na chini ni Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kushoto) akitoa maelezo ya shughuli mbalimbali za utalii na vivutio vyake nchini Tanzania kwa baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali vikiwemo vya utalii nchini Zimbabwe waliofika katika banda la Tanzania kwenye maonyesho ya nane ya Kimataifa ya Utalii Sanganai/Hlanganani–(World Tourism Expo) kupata taarifa mbalimbali za vivutio vya utalii wa Tanzania yaliyomalizika jana jijini Harare katika ukumbi wa hoteli ya Rainbow Towers.
(Picha zote na Zainul Mzige wa

IMG_4137
Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kulia) akibadilishana mawazo na wananfunzi wa Belvedere Technical Teachers College nchini Zimbabwe, Francisca Chipuriro (kushoto) na Natalie Takavarasha (katikati) wakati walipotembelea banda la Tanzania kwa ajili ya kupata taarifa mbalimbali za utalii wa Tanzania na vivutio vyake siku ya ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo yaliyomalizika juzi jijini Harare katika hoteli ya Rainbow Towers.
IMG_4185
Wageni mbalimbali waliovutiwa na vivutio vya utalii nchini Tanzania wakiendelea kumiminika katika banda la Tanzania na kupata taarifa mbalimbali kutoka kwa Afisa Habari Mwandamizi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Esther Solomon (kulia) ambapo hivi sasa Shirika la ndege la Fastjet limeanza safari zake jijini Harare kupitia Lusaka hadi Dar es Salaam kwa gharama nafuu kabisa itakayowezesha wananchi wa Zimbabwe kufanya safari za Tanzania kwa gharama nafuu kabisa.

No comments:

Post a Comment