MAHAKAMA
ya wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, imemtia hatiani na kumhukumu
Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe kwenda jela mwaka mmoja au
kulipa faini ya Sh milioni moja, kutokana na kesi iliyokuwa ikimkabili
ya kumshambulia mwangalizi wa ndani wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010.
Akisoma
hukumu hiyo iliyohudhuriwa na wabunge wengi wa Chadema, Hakimu Mkazi
Mfawidhi, Denis Mpelembwa, alisema mahakama imemkuta Mbowe na hatia,
hivyo kutakiwa kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini
kiasi cha Sh milioni moja.
Mbowe
ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hai, katika kesi hiyo ya jinai namba 73
ya mwaka 2011, alidaiwa kumshambulia Nassir Yamin, katika Kijiji cha
Nshara, kata ya Machame Kaskazini, Wilaya ya Hai, katika uchaguzi mkuu
wa mwaka 2010. Mpelembwa alisema mahakamani hapo kuwa hukumu iliyotolewa
mahakamani hapo imezingatia ushahidi uliotolewa kwa upande wa
mlalamikaji Nassir Yamini.
No comments:
Post a Comment